Jose MourinhoImage copyrightAGES
Image captionJose Mourinho alitumikia marufuku ya mechi moja dhidi ya Swansea chini ya mwezi mmoja uliopita
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anakabiliwa na uwezekano wa kuadhibiwa tena na Chama cha Soka Uingereza (FA) baada ya kufukuzwa uwanjani na refa Jumapili.
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwake kufukuzwa uwanjani na mwamuzi katika kipindi cha mwezi mmoja.
Mreno huyo alifukuzwa na mwamuzi Jon Moss baada yake kuonekana kukerwa na uamuzi wa refa huyo wa kumuonesha Paul Pogba kadi ya manjano kwa kujiangusha uwanjani mechi ya dhidi ya West Ham, na akapiga chupa teke kwa hasira.
Mechi hiyo ilimalizika sare 1-1.
Video zinaonesha mchezaji wa West Ham Mark Noble hakumgusa Pogba hata kidogo.
Mourinho, pia alifukuzwa uwanjani mwezi uliopita na refa Mark Clattenburg wakati wa mechi iliyomalizika sare 0-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Burnley.
Alitumikia marufuku ya mechi moja wakati wa mechi dhidi ya Swansea.
Katika kisa kingine, alitozwa faini ya £50,000 kwa tamko lake kuhusu mwamuzi Anthony Taylor kabla ya mechi kati ya Manchester United na Liverpool.
Moss pia alimfukuza uwanjani Mourinho Oktoba 2015 Mreno huyo alipokuwa anaikufunza Chelsea wakati wa mechi dhidi ya West Ham.
Mourinho akipiga chupa teke wakati wa mechi dhidi ya West HamImage copyright
Image caption

0 comments :

Post a Comment

 
Top
Godysamtz.blospot.Com