Kocha Mkuu wa timu ya Simba Mganda, Jackson Mayanja, ametamba na kusema ubingwa msimu huu utatua mitaa ya Msimbazi huku akiwataka wapinzani wao Yanga kuusahau kwani wamedhamiria kufanya hivyo kwa vitendo.
Mayanja alitoa tambo hizo juzi mara baada ya kumalizika mechi yao na timu ya Coastal Union ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani.
Alisema ushindi huo umewapa nguvu kubwa ya kuendeleza mapambano kwenye michezo yao inayofuata ili waweze kutimiza azma yao ya kuweza kuchukua ubingwa hasa ukizingatia kasi waliyokuwa nayo haiwezi kukamatwa na timu yoyote ile.

Aidha, alisema licha ya kupata ushindi wanakwenda kujipanga na kujiimarisha zaidi kwa ajili ya michezo yao inayofuata kwenye michuano ya Ligi Kuu soka Tanzania.

“Huu moto ambao tumekuwa tukiuwasha kwenye mechi zetu za lig si wa kuzimwa na timu yoyote ile mpaka tuchukue ubingwa na hiyo ndiyo dhamira yetu kubwa msimu huu,” alisema.


Wakati huo huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alionekana kuwa kivutio kikubwa baada ya mchezo baina yao na Coastal Union ambapo alisimama juu na kuingia uwanjani kuanza kucheza.

Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

0 comments :

Post a Comment

 
Top
Godysamtz.blospot.Com